Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge yashauri Vijana wa Kike kujikita katika fani ya Umeme wa Magari


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq ametoa wito kwa Uongozi wa Chuo cha St. Anton Vocational Training Center Musoma kuwahimiza Vijana wa kike kujikita katika fani ya umeme wa magari.

Mhe, Toufiq amebainisha hayo leo Machi 14, 2024 waliopo fanya ziara katika chuoni hapo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi Nchini inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Aidha, amesema kumekuwepo na idadi ndogo ya vijana wa kike wabobevu katika fani hiyo hali ambayo inapunguza ushindani katika soko la Ajira..

Kwa upande wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewahimiza wanafunzi wa chuo hicho kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo ya Rais Samia ya kuona umuhimu wa kuwekeza kwa vijana.

Naye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika ofisi hiyo, Saidi Mabie amesema hadi sasa serikali imetoa Milioni 65 kwa wanafunzi 140 ambao wanasomeshwa bila malipo yoyote chuoni hapo.

Awali akisoma hutuba kwa Kamati hiyo Mratibu wa Programu ya Kukuza Ujuzi na Mwalimu wa Taaluma katika Chuoni hapo Petronila Shirima ameiomba Serikali kuwafadhili vifaa Watu wenye ulemavu mara baada ya kumaliza masomo yao ili waweze kujimudu kimaisha.