Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Hakuna Usafirishaji Haramu wa Watoto na Watu Wenye Ulemavu Namanga - Mhe. Katambi


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amethibitisha kutokuwepo kwa usafirishaji haramu wa biashara ya binadamu katika mpaka wa Namanga na Kenya hususani kwa watoto na wenye ulemavu.

Mhe. Katambi amethibitisha hayo Januari 3, 2023 Jijini Arusha katika Wilaya ya Longido alipofanya ziara katika mpaka wa namanga kwa ajili ya kukagua hali ya utoaji huduma kwa abiria.

Amesema taarifa ambazo hivi karibuni zimesambazwa katika mitandao ya kijamii juu ya watoto na wenye ulemavu kusafirishwa kinyume na sheria na kupelekwa nchini kenya kwa ajili ya kutumikishwa zipuuzwe kutokana na hali ya ulinzi na usalama uliopo katika mpaka huo.

Ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kudhibiti vipenyo visivyo halali ikiwa ni pamoja na kuweka polisi jamii ili kuwachukulia hatua watakao bainika wanapita bila kufuata utaratibu.

Aidha, amesema Serikali ya Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mfumo wa kielekroniki wa kupata hati ya kusafiria kwa muda mfupi hivyo hakuna sababu ya kusafiri bila kufuata utaratibu.WhatsApp%20Image%202024-01-03%20at%2022.45.14-3