Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ridhiwani Kikwete ashiriki katika shughuli za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa hadhara na wakazi wa Mkoa wa Pwani ambao umefanyika Aprili 25, 2025 katika stendi ya Kibaha ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Aidha, Mgeni rasmi katika Mkutano huo alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

Akizungumza na Wananchi wa Mkoa huo, Mhe. Tulia amewahimiza wananchi kulinda na kuendelea kuuenzi Muungano ulioanzishwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Aman Abeid Karume.

“Tanzania haiwezi kuwepo bila Muungano, Muungano huu umejengwa katika misingi imara na umedumu, hivyo kila mmoja wetu anawajibu kuwa chachu ya kudumisha Muungano huu” amesisitiza Dkt. Tulia

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuenzi muungano kwa kushirikiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

"Muungano wetu umeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar," amesema