News
Waziri Kikwete afungua Kongamano Maalum la Wafanyakazi Mkoani Singida
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amefungua kongamano maalum la Wafanyakazi kuelekea siku ya Wafanyakaazi Duniani, leo Aprili 28, 2025 Mkoani Singida.
Aidha, Mhe. Ridhiwani amewapongeza wafanyakazi, waajiri, na Serikali kwa ujumla kwa maandalizi mazuri yanayoendelea kufanyika kwa ajili ya kufanikisha sherehe za Mei Mosi za mwaka huu wa 2025 na hasa maandalizi ya kongamano hilo.
Kongamano hilo lilikuwa na mada isemayo “Ushirikiano kati ya Serikali, Waajiri na Wafanyakazi katika Kuleta Tija Mahali Pa Kazi”