Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Waziri Sangu akutana na Bodi ya Uongozi ATE


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu (MB), tarehe 13 Disemba 2025, amekutana na kuzungumza na Wajumbe wa Bodi ya Uongozi Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wakati wa Mkutano wa 72 wa Bodi ya Uongozi uliofanyika katika Hoteli ya Seacliff, Dar es Salaam.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Wajumbe wa bodi wanaowakilisha sekta mbalimbali, Bi. Caroline Mugalla, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Wanachama wa ATE kutoka NMB Bank, Chemi Cotex, ALAF, TSIA, Heritage Insurance.

Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Deus Sangu alitolea ufafanuzi kuhusu dhana ya Mahusiano katika Wizara. Pia alisisitiza kuwa alisisitiza kuwa Waajiri ndio injini ya uchumi, wanaozalisha ajira, kulipa kodi, kuwekeza na kuchochea ukuaji. Pia alisisitiza maeneo muhimu yanayohitaji maboresho na kuahidi kushurikiana na Waajiri kuyafanyia kazi huku akisisitiza Waajiri kufuata Sheria za kazi na kulinda haki za wafanyakazi.

Katika mkutano huo, Mhe. Sangu pia alizindua Mpango Mkakati wa ATE 2026–2030, na kuwapongeza ATE kupanga mikakati yao sambamba na Dira ya Taifa 2050.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bw. Oscar Mgaya, alisisitiza dhamira ya ATE kuendelea kusimamia maslahi ya Waajiri na kuchangia katika sekta ya ajira na kazi ili kuleta tija na ushindani.