Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Dkt. Biteko asisitiza umuhimu wa Elimu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi


*Aipongeza OSHA kuboresha utendaji*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameitaka OSHA kuendelea kutoa elimu ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi kwa kushirikiana na wadau katika masuala ya Usalama mahali Pa kazi ili kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na mazingira yatakayowawezesha kuwa salama na kuwezesha kuongeza tija katika uzalishaji.

Dkt. Biteko amesema hayo (leo Aprili 28, 2024) Jijini Arusha katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi Duniani.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi amebainisha kuwa serikali inaendelea kushirikiana na wadau wa utatu ikiwa ni Waajiri na Wafanyakazi katika kuhakikisha Tanzania inazingatia Usalama na afya mahala Pa kazi.

Mkurugenzi wa Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bi. Caroline Mugalla ameipongeza Serikali kwa kuendelea na michakato ya kuridhia mikataba miwili ya ILO kupitia makubaliano ya pamoja baina ya Wafanyakazi na Serikali ili kuleta ufanisi mahali pa kazi na ameahidi ILO kutoa ushirikiano kwa serikali.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri (ATE) ametoa wito kwa Serikali na Waajiri kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa inayozingatia usalama na afya mahala pa kazi.

Aidha, Mwakilishi wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Bi. Juliana Mpanduji amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali kupitia OSHA na ATE ili kulinda nguvu kazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.