Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Bodaboda changamkieni asilimia 10 ya Mkopo: Ndejembi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amewahimiza Maafisa Usafirishaji (Boda Boda) Mkoani Arusha kuchangamkia asilimia 10 ya Mkopo kwa Wanawake, Vijana na Makundi maalumu ili kuongeza tija na uzalishaji katika kazi zao.

Mhe. Ndejembi amebainisha hayo Aprili 29, 2024 Mkoani humo wakati akihitimisha Mafunzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa boda boda ambapo amewasisitiza kufuata taratibu za kupata mkopo huo ikiwemo kuwa na leseni ya uendeshaji pikipiki.

Aidha, amewasisitiza kufanya kwa usalama wakizingatia kanuni, sheria na miongozo iliyowekwa na serikali ili kuepukana na ajali zinazojitokeza na kupelekea vifo na ulemavu wa kudumu.

Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Boda Boda Mkoani humo Okero Costantine ameipongeza OSHA kwa mafunzo waliyoyatoa na amesema elimu waliyoipata itapunguza asilimia kubwa ya ajali.