Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ridhiwani ashiriki Mafunzo ya OSHA kwa Watendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kati


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki katika mafunzo ya usalama na afya kwa Watendaji wa Mahakama Kuu - Kanda ya ya Kati yaliyofanyika Aprili 23, 2025 katika ukumbi wa mikutano jengo la OSHA, Jijini Dodoma.

Aidha, Mafunzo hayo yalifunguliwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema mafunzo hayo yanayotolewa na OSHA ni utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya Mwaka 2003 ambayo inaitaka Wakala huo kutekeleza wajibu wa kulinda usalama na afya za wafanyakazi.

"Mafunzo haya yatasaidia kuwajengea uelewa wa namna ya kubaini vihatarishi katika maeneo yenu ya kazi na kudhibiti ili visilete madhara kwa wafanyakazi," amesema

Mafunzo hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo "Nafasi ya Teknolojia na Matumizi ya Akili Unde Mahali pa Kazi (Mapinduzi na Fursa)"

Katika mafunzo hayo pia wameshiriki viongozi mbalimbali akiwemo Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu - Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose Mlyambina, Mtendaji Mkuu OSHA, Khadija Mwenda, Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa na Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Usekelege Mpulla.