Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI MHAGAMA AZIAGIZA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI KUKUMBUKA WATU WENYE WALEMAVU


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ameziagiza Taasisi za Umma na binafsi kukumbuka kundi la watu wenye ulemavu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiangalia jinsi mmoja wa wanafunzi anavyotumia mashine maalumu ya kuandikia. (Kulia ni) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa

Waziri Mhagama aliyasema hayo Septemba 17, 2018 wakati alipokuwa akipokea mashine maalum za kuandika kwa wanafunzi wasioona (Braille Machines) kutoka Mfuko fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye Chuo cha Walemavu Yombo, Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mhagama aliambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Wenye Ulemavu. Naibu Waziri Ikupa amewasii watu wenye ulemavu nchini kujiamini, kujitambua, kujikubali na kuongeza bidii katika kazi wanazofanya.