News
Vikundi Kazi Kinga ya Jamii Vyazinduliwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mary Maganga ametoa wito kwa vikundi kazi (Thematic Working Group) vilivyojikita katika maeneo makuu manne (Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Uchangiaji; Huduma za Misaada ya Kijamii; Huduma za Uzalishaji Shirikishi na Huduma za Ustawi wa Jamii) kufanya kazi kwa weledi na kutekeleza Mfumo wa Kinga ya jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa vikundi kazi hivyo leo Januari 20, 2025 jijini Dodoma Maganga amesema kuwa Vikundi kazi vitachangia kuimarisha mpango wa Kitaifa wa Kinga ya Jamii kwa kuhakikisha kuwa makundi yaliyo mengi katika jamii yanafikiwa na kupata huduma zinazofaa, lakini pia ni hatua muhimu katika kutoa muelekeo wa kuleta mabadiliko ya kudumu katika mfumo wa jamii.
“Kupitia vikundi hivi tutaweza kujenga msingi thabiti wa ustawi wa jamii yetu ambapo hakuna mtu atakae saulika au kubaguliwa”, amesema