Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ukusanyaji Maoni ya Sera Mpya ya Watu wenye Ulemavu mbioni kukamilika


Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imesema zoezi la ukusanyaji maoni ya mapitio ya Sera Mpya ya Watu Wenye Ulemavu lipo mbioni kukamilika ili kuleta ustawi bora kwa watu hao.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu wa Ofisi hiyo, Rasheed Maftah ameyasema hayo Oktoba 5, 2023 alipokutana na kundi la watu wenye ulemavu jijini Dodoma kwa lengo la kupata maoni ya mapitio ya sera hiyo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa zoezi hilo limehusisha mikoa yote ya Tanzania bara na kwa sasa lipo hatua za mwisho za kukamilika mkoani Dodoma ambapo makundi yote yameshirikishwa.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma Andrew Method ameeleza kuwa maboresho yanayotakiwa kuzingatiwa ni kuhakikisha inaendana na mabadiliko ya teknolojia, uwezeshaji kiuchumi kwa wenye ulemavu, vipaumbele vya ajira na miundombinu wezeshi kwa kundi hilo.

Mmoja wa mtoa maoni, Bwire Manoko ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali na kuwasikiliza kundi la Watu Wenye Ulemavu na kuwapa kipambele kwenye mahitaji yao.