News
Ridhiwani: Rais Samia anawapenda Wenye Ulemavu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawapenda na kuwajali Watu Wenye Ulemavu.
Amebainisha hayo Desemba 15, 2024 Jijini Dodoma katika mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qura'n tukufu kwa Wenye Ulemavu.
Aidha, Mhe. Ridhiwani ametumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi kuendelea kuwasomesha Wenye ulemavu Qur, an tukufu ili waweze kukua katika maadili ya kumpendeza mungu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Rizick Lulida (Mb)