Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Pro.Ndalichako aridhishwa na Mandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekagua na kuridhishwa na shughuli za maandalizi ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 Mkoani Manyara.

Prof. Ndalichako amefanya ukaguzi huo Oktoba 2, 2023 alipofanya ziara Mkoani humo ambapo ametoa pongezi kwa Mkoa huo kwa kujenga uwanja wa kisasa ambao utatumika katika shughuli za kilele cha mbio za mwenge pamoja na michezo.

Aidha, ametoa rai kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala nchini kuhakikisha wanawafikisha vijana Mkoani humo ili kupata fursa ya kuuza bidhaa zao, kuonesha ubunifu, kutengeneza masoko na kupata uzoefu wa namna ambavyo vijana wengine wanafanya kazi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa wito kwa vijana kufika Mkoani humo kuanzia Oktoba 8 hadi 14 ili kushiriki mijadala mbalimbali ya kuwainua vijana kiuchumi ikiwemo fursa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Naye Mkuu Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema kila eneo ambalo limepangwa kwa ajili ya shughuli za kilele cha mbio za mwenge zipo mbioni kukamilika ambapo ifikapo Oktoba 6, 2023 maeneo yote yatakuwa yamekamilika.