Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mwenge wa Uhuru waweka Jiwe la Msingi Zahanati ya Kimashuku


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Bw. Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kimashuku leo Aprili 3, 2024 na kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Hai kwa usimimizi mzuri wa mradi huo.

Aidha, Bw. Mnzava amesisitiza manunuzi ya serikali yafanyike katika mfumo wa NesT na kuijengea uwezo kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, watendaji na wasimamizi wote wanaotoa huduma za afya kutekeleza sheria ya manunuzi.

Akisoma taarifa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mganga mfawidhi wa wilaya ya Hai Dkt. Itikija Msuya, amesema mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 117,500,000.00 hadi kukamilika ambapo kwa sasa umetumia kiasi cha shilingi Milioni 76,214,168.00 kimetumika na umetoa ajira kwa wananchi 40.

Zahanati hiyo inatarajiwa kihudumia wananchi 5,367 na kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje, klinik ya baba, mama na mtoto pamoja na kutoa huduma nyingine.

Hata hivyo, Mnzava ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa kutoa zaidi ya Shilingi Mil 650 kwa ajili ya Ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Majengo.

“Tumejiridhisha na mradi huu baada ya kuukagua na kupitia nyaraka za mradi huu tumebaini zipo vizuri. Nikiri mpaka hatua hii kazi kubwa na nzuri imefanyika hivyo Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 tumeridhia uwekaji jiwe la msingi katika mradi huu" alisema Mnzava.