News
Mhe. Ridhiwani akagua maandalizi sherehe za Mei Mosi 2025 Singida
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Aprili 22, 2025 amekagua maendeleo ya ukarabati uwanja wa Bombadia Mkoani Sindida ambapo maandimisho ya sherehe za Mei Mosi kwa mwaka huu zitafanyika.
Aidha, akiwa katika ukaguzi huo Mhe. Ridhiwani ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Vicent Mashinji, Mkuu wa Wilaya Singida Mhe. Godwin Gondwe, Kamishna wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu Suzan Mkangwa, viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na viongozi wa Mkoa huo.