Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe.Katambi ataka Vijana wajasiriamali kupatiwa ithibati za bidhaa kwa wakati


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutoa ithibati ya bidhaa wanazozalisha Vijana wajasiriamali kwa wakati ili kuwaendeleza na kukuza uchumi wa Taifa.

Mhe. Katambi ametoa agizo hilo Oktoba 5, 2023 Jijini Dodoma wakati akifunga mdahalo kuhusu vijana na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo ulioandaliwa na bodi ya wadhamini na Menejimenti ya Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko (AMDT).

Amesema katika maeneo mengi ambayo ametembelea, TBS imekuwa ikilalamikiwa kutowafikia vijana wajasilimali kwa wakati na kutoa mashariti magumu ambayo yanachukua muda mrefu hivyo watoe elimu ya namna ya kufikiwa ili bidhaa wanazozitengeneza zipatiwe vipimo kwa wakati.

Aidha, Mhe. Katambi amesema Serikali imeanzisha mafunzo ya kilimo cha kisasa ambapo jumla ya Vijana 13,088 wamepatiwa mafunzo kati yao vijana 12,580 ni wa mafunzo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba, vijana 234 ni wa mafunzo ya kunenepesha mifugo, vijana 200 ni wa mafunzo ya ufugaji samaki na viumbe maji, na vijana 74 ni wa kilimo cha mazao kwa njia ya vizimba.