Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhandisi Luhemeja: Tufanye kazi kwa ushirikiano na kutangaza mafanikio yetu


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, leo tarehe 15 Disemba, 2023, amefanya kikao kazi na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali zikiwa zimetimia siku 100 tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kikao kazi hicho kilifanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma, na kimehudhuriwa na watendaji kutoka NSSF, PSSSF, WCF, CMA, OSHA,RTU, DSS na Idara ya Kazi na Idara ya Maendeleo ya Vijana.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Luhemeja aliwataka watendaji wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zilizo chini yake kufanyakazi kwa ushirikiano, kuwa wabunifu, kuongeza juhudi ya kazi, kutatua kero za wananchi pamoja na kutangaza mafanikio makubwa ambayo Ofisi hiyo na Idara zilizo chini yake imeyafanya.

Mhandisi Luhemeja amesema mambo mazuri yaliyofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Idara zilizo chini yake yanapaswa kutangazwa ili wananchi waweze kuyafahamu na hiyo ndio dira ya Serikali.