Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Katibu Mkuu Maganga apongeza Baraza la Wafanyakazi OSHA


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mary Maganga amewataka wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia usawa ili kuongeza tija hatua itakayochochea kufikia malengo ya Taasisi.

Akifungua kikao cha Tano cha Baraza la Wafanyakazi wa OSHA, jijini Dodoma (20 Desemba 2025) chenye lengo la kuthathimni utendaji wa Taasisi ilipo na inapokwenda,Katibu Mkuu huyo alisisitiza ushirikiano kama nguzo ya kufikia mafanikio ya Taasisi.

Bi. Maganga amewaasa wafanyakazi kuwafundisha maadili ya kazi wafanyakazi wageni na wapya kwenye ajira ili kuendeleza mnyororo wa kufanya kazi kwa weledi na kufikia malengo ya taasisis kwa wakati.

Awali akizungumza Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda amesema kikao hicho kinalenga kutathmini utendaji wa Taasisi ya OSHA kwa kutazama kipindi kilichopita, kilichopo ili kupata mustakabali wa maendeleo ya OSHA katika kipindi kijacho.

“Kikao hiki pamoja na kutathmini utendaji wa Taasisi kwa mwaka wa fedha uliopita (2024/2025) kinalenga kuangalia mwenendo wa utendaji wetu katika miezi mitano iliyopita ya mwaka huu wa fedha (2025/2026) hususan katika kipindi hiki tunapoelekea kuandaa bajeti ya mwaka wa fedha ujao (2026/2027),” amesema Mtendaji Mkuu.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) ambacho wafanyakazi wa OSHA ni miongoni mwa wanachama wake, Bw. Rugemalila Rutatina, ameipongeza OSHA kwakuwa na utaratibu mzuri wa ushirikishwaji watumishi wote pasipo ubaguzi katika kufanya maamuzi ya masuala muhimu yanayohusu utendaji wa Taasisi hiyo.