Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndejembi ateta na Mwakilishi Mkazi UNFPA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner yanayolenga kuimarisha ushirikiano kwenye maendeleo ya vijana na watu wenye ulemavu.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Juni 27, 2024 jijini Dodoma ambapo Mhe. Ndejembi amemhakikishia Bw. Schreiner kuwa Tanzania itahakikisha kundi kubwa la vijana linashiriki katika mkutano wa vijana (Youth Connect) utakaofanyika Novemba mwaka huu Kigali, nchini Rwanda.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Bw. Rasheed Maftah, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana, Bw. Godfrey Massawe pamoja na wataalamu wengine kutoka UNFPA.