Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndejembi ashiriki Mkutano wa 112 ILO


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Mhe Deogratius Ndejembi ameshiriki mkutano wa 112 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambao unafanyika jijini Geneva, Uswisi.

Mkutano huo unakutanisha Nchi wanachama wa ILO kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya haki ya mfanyakazi mahala pa kazi.

Wengine walio hudhuria mkutano huo ni ; Kamishna wa Kazi, Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Viongozi wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) pamoja na Mahakama Divisheni ya Kazi.