Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndejembi ashiriki makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Julai 05, 2024 ameshiriki zoezi la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa kutoka Mkoa wa Dodoma kuelekea Mkoa wa Singida.

Zoezi hilo limefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego na kushuhudiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2024, Ndugu Godfrey Eliakim Nzava.