News
Waziri Mkuu aridhishwa na maandalizi kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2024
WAZIRI Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameridhishwa na maandalizi ya maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yatafanyika mkoani Mwanza, Oktoba 14, 2024.
Amesema hayo leo Oktoba 13, 2024 wakati akikagua maandalizi hayo ambayo yatafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
“Nimeridhishwa na maandalizi na niwapongeze kwa kukamilisha shughuli zote za maandalizi haya," amesema
Awali akitoa taarifa ya maandalizi hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema maandalizi yamekamilika na hamasa kubwa imefanywa na Mkoa wa Mwanza katika kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan