Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Watoa Huduma Sekta ya Hoteli wapigwa msasa


Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yawapiga msasa watoa huduma katika sekta ya hoteli ili kutoa huduma bora kwa watalii wa nje na ndani ya nchi.

Aidha, Watoa huduma zaidi ya 350 wamepata mafunzo hayo, huku yakihudhuriwa na watoa huduma wa Uandaaji wa chakula (Food Production), Huduma ya Chakula na Vinywaji (Food&Beverage), Uandaaji wa Vyumba (House Keeping) na Mapokezi (Front Office).

Kadhalika, Watoa huduma hao wamepatiwa ujuzi wa ukarimu huduma kwa wateja (Hospitality Customer Care) na Huduma ya Kwanza ili kumuwezesha mtoa huduma kupata uelewa wa kuweza kufanya usaidizi wa awali wa kuokoa maisha kabla ya mgonjwa kufikishwa kwenye huduma ya afya.