News
Wakulima wa Zabibu wapigwa msasa Kilimo cha tija
Wakulima wa zao la Zabibu kutoka katika Vyama vya Msingi vya Ushirika mkoani Dodoma wamepata mafunzo ya stadi za kilimo cha tija kwa zao la zabibu leo Oktoba 17, 2024 Jijini Dodoma.
Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Kitengo cha Ukuzaji Tija na Ubunifu yamejikita katika kuwawezesha wakulima hao kushiriki katika kilimo chenye tija na ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi . Aidha; wakulima hao wamepata mafunzo juu ya Ujasiriamali.