News
Wadau Wizara za Kisekta watakiwa kuwa mabalozi wa ukuzaji tija na ubunifu
Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Yohana Madadi amewataka wadau kutoka wizara za kisekta kuwa mabalozi wa ukuzaji Tija na Ubunifu nchini.
Akifungua kikao kazi cha Maboresho ya Programu ya kukuza Tija na Ubunifu nchini na mwongozo wa kupima Tija kwa wadau wa Tija na Ubunifu, leo Oktoba 16, 2024 Jijini Dodoma, Kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu wa ofisi hiyo amewasisitiza washiriki wa kikao hicho kuwa mabalozi wazuri katika utekelezaji wa programu ya Ukuzaji Tija na Ubunifu nchini
Aidha, katika hatua nyingine washiriki wa kikao kazi hicho wametoa maoni katika kuboresha programu hiyo na Mwongozo wa kupima tija nchini ili kuweza kupata matokeo yaliyokusudiwa.