Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wadau wa utatu wajadili Program ya Taifa ya Kazi za Staha


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri ya Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Shirika la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), ATE na Mashirika ya maendeleo wamekutana leo Aprili 14, 2025 jijini Dodoma katika kikao cha wadau wa utatu ili kujadili kuhusu Programu ya Taifa ya Kazi za Staha Awamu ya Tatu.

Akifungua kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus ameshukuru shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kuendelea kushirikiana na serikali kusimamia programu hiyo ambayo ina lenga kuwezesha nchi wananchama ikiwemo Tanzania katika kukuza kazi za staha.

Aidha, amesema mpango huo wa tatu wa programu hiyo utaiwezesha ILO kusaidia nchi wananchama kutekeleza afua mbalimbali zinazojumuisha ukuzaji ujuzi, kinga ya jamii na majadiliano ya Pamoja sehemu za Kazi.

Naye Afisa Mwandamizi wa Programu (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Edmund Moshy amesema shirika hilo lipo tayari kushirikiana na serikali ili kutimiza mpango wa tatu wa programu ya Taifa ya Kazi za Staha ambao utakuwa nyenzo Madhubuti ya kukuza fursa za ajira zenye tija, hifadhi ya jamii haki kazini na majadiliano ya kijamii.