Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waajiri sekta ya utalii waaswa kuzingatia sheria za kazi


Waajiri sekta ya utalii nchini wametakiwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kutoa mikataba kwa wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi.

Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Suzan Mkangwa wakati wa semina ya siku mbili kwa wadau wa sekta ya utalii iliyofanyika Jijini Arusha.

Amesema lengo la semina hiyo ni kutoa elimu ya kutambua wajibu wao katika kutekeleleza sheria za kazi na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii nchini.

”Baada ya semina hii tunaamini mambo mengi yataenda kubadilika na sekta hii itaendelea kuimarika kwa kufuata sheria za kazi” amesema

Wakizungumza kwa nyakati tofauti waajiri na wafanyakazi walioshiriki katika semina hiyo wamesema kuwa elimu waliyopata kuhusu sheria za kazi itasaidia kupunguza migogoro ya kikazi na kuhakikisha waajiri na wafanyakazi wanatii sheria katika maeneo ya kazi.