Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waajiri nchini wahimizwa kuhamasisha matumizi ya teknolojia kazini


SERIKALI imewataka waajiri nchini kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika sehemu za kazi lakini pia kuandaa watalaam kwenye eneo la digitali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira & Wenye Ulemavu ) Patrobas Katambi alisema hayo jana Dar es Salaam katika mkutano wa mwaka wa 65 wa ATE na kuongeza kuwa iko tayari kushirikiana na sekta binafsi ikiwemo Chama cha Waajiri nchini (ATE) kuhakikisha matumizi ya teknolojia.

Aidha, Mhe. Katambi amesema ni lazima kama Taifa kwenda na mabadiliko ya teknolojia lakini muhimu kulinda misingi ya nchi ikiwemo kuwa na miundombinu ya uwezo wa teknolojia hizo, elimu na ujuzi, mifumo wa sheria na sera nzuri.