Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi watakiwa kuwa chanzo cha utulivu katika vyama vyao


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kuwa chanzo cha utulivu katika vyama vyao ili kuepuka migogoro ambayo inaweza kuathiri utendaji kazi sehemu za kazi.

Mhe. Ndejembi amesema hayo leo Julai 05, 2024 Jijini Dodoma alipokutana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi vya TUGHE na TALGWU ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili masuala mbalimbali ya kiutendaji ya vyama hivyo pamoja na changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mary Maganga.