Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Taasisi ya Young Life Tanzania


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Taasisi ya Young Life Tanzania ili kuhakikisha inatimiza malengo ya vijana ikiwemo kuwainua kiuchumi.

Mhe. Katambi amebainisha hayo leo Julai 15, 2024 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kusherekea Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ambayo inajihusisha na kuwalea vijana katika maadili ya kiroho na kuwa viongozi bora katika Taifa lao..