Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali imezalisha Ajira 8,084,204: Mhe. Majaliwa


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha Novemba 2020 hadi Februari, 2025 Serikali imefanikiwa kuzalisha ajira 8,084,204 katika sekta ya umma na sekta binafsi.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo leo Aprili 9, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa Fedha 2025/2026.

Aidha, amesema Serikali imeendelea kubuni na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuzalisha fursa za ajira nchini kupitia uwekezaji na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki, reli ya kisasa, Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato.

Kwa upande mwingine, Mhe. Majaliwa amebainisha kuwa katika kukuza mamaendeleo ya vijana nchini serikali ya awamu ya sita, imeendelea kuweka mazingira rafiki ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kujipatia ajira na kujikwamua kiuchumi.