Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Rais Samia Awataka Wasanii Kuwashawishi Vijana Kupenda Kilimo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amezindua jukwaa la Mfumo wa chakula Barani Afrika ambapo amewaomba wasanii kutumia vipaji vyao kuimba nyimbo na kufanya matangazo na kampeni mbalimbali za kuwashawishi Vijana wa kiume kuingia kwenye kilimo.

Rais Samia ameyasema hayo, Ikulu Dar es Salaam wakati akizindua Jukwaa AGRF, pamoja na kutangaza mkutano utafanyijka Septemba 5-8 nchini.

Katika uzinduzi huo umesema Tanzania ina fursa ya ardhi yenye rutuba na vyanzo vya maji hivyo vikitumika ipasavyo, ni wazi sekta ya kilimo itachochea pato la taifa kukua kwa kasi.

Amesema kilimo kinachangia uchumi wa Tanzania kwa asilimia 25 ambacho ni muhimu katika kukuza maendeleo, hivyo jitihada zake ni kuona mchango huo unaongezeka kwa kasi kubwa.

"Ombi langu Kwa wasanii, nimeambiwa wasanii mko hapa, Mrisho Mpoto nimemuona, wengine simameni, nilipokuwa sijaja hapa nimemuona mwanangu Alikiba yupo hapa na wengine na wengine, huko nyuma tulipokuwa na kampeni za kilimo ni wasanii waliohamasisha kampeni zile, nyimbo mbalimbali, michezo na matangazo Naomba mkatuunge mkono hapa pia"

"Mrisho Mpoto ameomba ubalozi na nina hakika ameshapewa Waziri yupo hapa lakini na wasanii wengine waliokuwepo hapa muende mkakae na Waziri muone vipi mtaweza kuwasaidia kuwafanya Vijana wenzenu waingie kwenye kilimo, muende mkawashawishi Vijana wenzenu wakaingie kwenye kilimo"

"Kilimo kimekuwa ni biashara ya wanawake kwa Sasa hivi hatuna shida tunajua wapo wanataka kuongezewa tu nguvu, mkawashawishi vijana pia"