Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Rais Samia ameendelea kuwezesha Vijana nchini: Mhe: Fatma Toufiq


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwezesha vijana na mafunzo ya ufundi na stadi za kazi kupitia programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo ina lenga kuimarisha nguvu kazi iliyo katika soko la ajira.

Amebainisha hayo leo Machi 15, 2025 alipoambatana na Wajumbe wa Kamati hiyo kwa ajili ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Don Bosco kilichopo Jijini Dar es salaam.

Mhe. Toufiq amesema mafunzo wanayopata vijana Chuoni hapo yanawasaidia kuwa na ujuzi ambao baada ya kuhitumu wanaweza kujiajiri na kuajiriwa na hivyo kuinua Uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kuendelea kuratibu Programu hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa vijana na kupunguza wimbi la Vijana wasio na ajira.

Akizungumza awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Alana Nchimbi amesema Programu hiyo ina lenga kuwezesha vijana kumudu ushindani katika soko la ajira kwa kuwawezesha kuajirika au kujiajiri.

Vile vile, amesema program hiyo imejikita pia kutoa mafunzo ikiwemo kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, Mafunzo ya vitendo mahali pa kazi kwa wahitimu na Mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi.