Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ndejembi: Mafao ya pensheni kwa wastaafu yanalipwa kwa mujibu wa sheria


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema mafao ya pensheni kwa wastaafu yanalipwa kwa mujibu wa sheria zinazosimamia Mifuko ya Hifadhi za Jamii ambapo zinaelekeza mifuko kulipa mafao ndani ya siku 60 tangu mwanachama anapostaafu.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Lushoto, Mhe Shabani Shekilindi aliyehoji ni lini Wazee wanaostaafu watapata mafao yao kwa wakati.

Vile vile, Waziri Ndejembi amesema kwa sasa mifuko ya hifadhi ya jamii imeboresha mifumo yao na wastaafu wote hulipwa mafao yao kwa wakati ndani ya siku 60.