Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ndejembi ashiriki uzinduzi ujenzi wa majengo pacha Kenya


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa majengo pacha ya kitega uchumi cha Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF), Nairobi nchini Kenya.

Aidha, Ujenzi wa mradi huo utakuwa na Ofisi za Ubalozi, Makazi ya Balozi na watumishi wa ubalozi wa Tanzania. Mradi huo umezinduliwa na Waziri Mkuu wa Kenya, Mhe Dkt Musalia Mudavadi ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Pia, katika uzinduzi huo amehudhuria Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe January Makamba pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Fatma Toufiq.