Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Naibu Mawaziri Katambi na Dkt. Mollel Wakabidhi Vyandarua kwa Wanawake Shinyanga


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Katika kuadhimisha siku ya Malaria Duniani, ameshirikiana na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kugawa vyandarua kwa wanawake zaidi ya 400 pamoja na kufikia makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Dkt Molel ameungana na mwenyeji wake katika Warsha iliyohudhuriwa na wanawake zaidi ya 400 ambayo imeratibiwa na Mhe. Katambi na kutekelezwa katika Manispaa hiyo kupitia Taasisi ya Doris Mollel na kufadhiliwa na AMREF.

Katika Warsha hiyo iliyofanyika Aprili 24, 2022, Shinyanga Mjini, Mhe. Katambi amefafanua kuwa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Huduma na miundo mbinu ya Afya katika Manispaa hiyo ambapo inakusudia kujenga Hospitali ya rufaa kwa wakati.

“Ilani ya Chama chama Mapinduzi imebainisha namna ya kumsaidia Mama na Mtoto, ujenzi wa Vituo vya Afya, lakini pia, Ilani inasisitiza namna ya kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuboresha huduma za Afya ambao kati ya hao ni Doris Mollel Foundation”

Naye, Dkt. Mollel alisema kuwa Serikali imelenga kuboresha huduma za uzazi, mama na mtoto na kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

"Asante wakina mama mliokuja hapa kupata elimu ili mkatusaidie kuelimisha wengine na kupunguza vifo vya akina mama na watoto" amepongeza Dkt. Mollel

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel Bi. Doris Mollel amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu ya ugonjwa malaria na namna ya kujikinga pamoja na kuhamasisha wanawake kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 ili waweze kujikinga janga hili kubwa la korona, tunaliona linaisha ila bado ugonjwa upo

"Zoezi limefanyika katika mikoa mitatu kwa kushirikiana na Amref kwa mikoa ya Simiyu, Kagera na Shinyanga na tunaishukuru Serikali kwa kutuwekea mazingira wezeshi sisi taasisi binafsi kuweza kufanya kazi na kutoa mchango wetu ndani ya jamii" amesema Doris Mollel.