Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Ridhiwani Kikwete ateta na Mwakilishi wa UN WOMEN TANZANIA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kuzungumza na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN WOMEN), anayeshughulika masuala ya kuwezesha na kutetea haki na usawa kwa wanawake, Hodan Addou, leo Machi 24, 2025 Jijini Dar es salaam.

Aidha, katika kikao hicho wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la umuhimu wa elimu katika kusaidia kundi la Watu Wenye Ulemavu hususan watoto wa kike na wanawake.

Aidha Mhe. Ridhiwani ameishukuru UN Women kwa kuendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kundi la Watu wenye mahitaji maalum linafikia malengo yao katika sambamba kushiriki kikamilifu katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa.

Awali akizungumza Mwakililishi wa UN Women Ms. Hodan Addou amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuyapa kipaumbele masuala ya Watu Wenye Ulemavu ili kukuza ustawi wa kundi hilo