Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Ndejembi: Serikali ni sikivu imeboresha Kikokotoo


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaguswa na maslahi ya wafanyakazi ambapo imechukua hatua ya kutenga Bilioni 155 kwa ajili ya kuboresha na kuongeza malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliyopo sasa hadi asilimia 40.

Pia, Kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33 sasa litakuwa likipokea asilimia 35.

Mhe Waziri Ndejembi ameyasema hayo leo wakati akichangia akichangia hoja yake Bungeni Jijini Dodoma katika Bunge la Bajeti ya Mwaka 2024/2025 linaloendelea.

Aidha, Mhe. Ndejembi amefanua kuwa, mabadiliko hayo hayatawahusu tu wanaostaafu kuanzia tarehe 1 Julai 2024 bali watanufaika wastaafu wote ikiwemo watumishi 17,068 waliostaafu kuanzia julai 2022 hadi juni 2024 ambao watalipwa mapunjo yao ya asilimia 7 na wale waliopanda asilimia 33 kwenda asilimia 35 watalipwa asilimia 2 ambayo wanastahili kupata.

Vile vile, Waziri Ndejembi amesema kuwa kadri mifuko ya hifadhi ya jamii inavyotengamaa ndivyo serikali itaendelea kufanyia kazi maboresho hayo zaidi.