Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Ndejembi ahamasisha Wananchi kuchangamkia fursa za uwezeshaji kiuchumi


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka wananchi kuchangamkia fursa za uwezeshaji kiuchumi na mikopo inayotolewa na serikali ili kujiinua kiuchumi na kuchangia katika pato la Taifa.

Amesema hayo leo Julai 10, 2024 jijini Dar es Salaam alipotembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba).

Mhe. Ndejembi amesema kuwa ushiriki wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake unalenga kutoa uelewa kwa umma kuhusu shughuli inazoratibu na fursa zinazotolewa na serikali ikiwemo suala la uwezeshaji makundi mbalimbali ya Vijana, Wananwake na Watu wenye Ulemavu.

Vile vile, Waziri Ndejembi amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki ya uwekezaji nchini, hivyo ametoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa ili waweze kunufaika wao binafsi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande mwengine, Mhe. Ndejembi amehimiza wanachi kutembelea banda hilo katika maonesho hayo ili kupata elimu na huduma zinazotolewa na ofisi hiyo.

Maonesho hayo ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji,”