News
Mhe. Katambi awahimiza Wanafunzi kuendelea kuuenzi Mwenge wa uhuru
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kibaha ambapo amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea kuuenzi Mwenge wa uhuru.
Uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa kwa mwaka 2025 unatarajiwa kuzinduliwa tarehe 2 Aprili 2025 katika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani.
Kauli mbinu ya mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 ni "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu"