Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Mhe. Katambi aeleza mikakati ya serikali kukuza lugha ya alama


*Abainisha matumizi ya Lugha ya Alama kusaidia kushirikisha na kujumuisha Viziwi kupata haki ya taarifa*

SERIKALI imeendelea kuchukua hatua stahiki kuhakikisha upatikanaji wa mawasiliano ya Lugha ya Alama kwa Watu wenye Ulemavu katika sekta mbalimbali ili kundi hilo liweze kupata haki ya taarifa.

Amesema hayo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakati akifungua mafunzo ya Lugha ya Alama kwa watumishi wa Suma JKT Guard, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Katambi amesema kuwa, Watu wenye Ulemavu wamekuwa hawapati huduma kikamilifu kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mawasiliano kwa watu wenye Uziwi.

"Jamii inapaswa kutambua ustawi wa Watu viziwi unatakiwa ujikitr katika upatikanaji wa mawasiliano ambapo lugha ya alama itasaidia kuboresha maisha yao," amesema

Vile vile, amebainisha kuwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo 2024 imeingiza tamko mahususi la kisera kwamba Serikali imeendelea kushirikiana na wadau, kuendeleza lugha ya alama, lugha ya alama Mguso na maandishi ya Breli katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

Kwa upande mwengine, Wanufaika wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yanawasaidi kuongeza tija katika utendaji wao wa kazi sambamba na kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo Watu wenye Ulemavu.

Naye, Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Rasheed Maftah amesema Sera ya huduma na Maendeleo kwa Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2004 inaelekeza umuhimu wa Lugha ya Alama ili kuhakikisha kwamba kundi la watu Viziwi basi wanaweza kuwasiliana kama ambavyo makundi mengi katika jamii yetu wanawasiliana kwa urahisi ili kuweza kupata haki na ustawi wao wa msingi ikiwemo huduma mbalimbali za afya, elimu, ulinzi na usalama.