Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Mhe. Katambi abainisha mikakati ya sekta ya uwezeshaji Vijana


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ameeleza kuwa Vijana wamekuwa wakiandaliwa kabla ya kupatiwa mikopo kwa kupitia mafunzo ya ujasiriamali, uanzishaji miradi, urasimishaji, usimamizi na uendelezaji shughuli zao.

Mhe. Katambi amebainisha hayo leo Mei 3, 2024 Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Prof. Patrick Ndakidemi (Mb) ambaye amehoji, Serikali inatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa kiasi gani kwa vijana kabla hawajapatiwa huduma za Mikopo toka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

Amesema vijana wamekuwa wakiunganishwa na huduma wezeshi kupitia taasisi za kifedha na benki, mamlaka za kodi, SIDO, huduma za udhibiti usalama na viwango (TBS, OSHA na TMDA) na huduma ya hifadhi ya jamii.

Vile vile, amesema Serikali ilianzisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa lengo la kuwapatia vijana mikopo yenye masharti nafuu ili kuwawezesha kuanzisha au kuendeleza miradi ya uzalishaji mali na kuwajengea vijana tabia ya kuweka akiba na kukopa kwa busara.

“Mfuko huu una majukumu makuu matatu ambayo ni Kutoa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo, Kutoa Mikopo na Kufanya Tathimini na Ufuatiliaji ikiwemo malezi kwa vijana waliokopeshwa (Mentorship)” amesema