News
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 kuzinduliwa Mkoani Pwani - Mhe. Ridhiwani Kikwete
✅ Wananchi wahamasishwa kujitokeza kwa wingi katika Uzinduzi huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Aprili 2, 2025 Mkoani Pwani.
Mhe. Kikwete amebainisha hayo leo Machi 26, 2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru ambapo amesema kuwa Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Aidha, Mhe. Ridhiwani ametoa wito kwa Wananchi wa Mkoa huo na Mikoa Jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Mkoani humo.
Amesema kuwa kauli mbiu ya Mwenge wa wa Uhuru 2025 inalenga kuwaelimisha na kuwakumbusha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu ambao utafanyika Oktoba Mwaka huu.
Vile vile, Waziri Ridhiwani Kikwete amesema Mwenge wa Uhuru 2025 utakimbizwa katika Mikoa 31 yenye jumla ya Halmashauri 195 nchini ikiwemo Bara na Visiwani, hivyo mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za Maendeleo.
Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ametembelea Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha ambapo uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kufanyika.