Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Matarajio ya Serikali kuona uzalishaji Kiwanda cha Mtibwa unarejea haraka


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema ni matumaini ya serikali kuona uzalishaji katika kiwanda cha sukari cha Mtibwa unarejea kwa haraka.

Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo Mei 26, 2024 alipofika katika kiwanda hicho ili kujionea mwenyewe hali halisi iliyopelekea ajali hiyo ya kupasuka kwa bomba la kusafirisha mvuke (steam) Mei 23, 2024 na kusababisha wafanyakazi 11 kufariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye wakiwa wanapatiwa matibabu hospitalini.

“Uzalishaji ukirejea haraka maana yake wafanyakazi watarudi kufanya kazi, na hivyo mtazalisha na sukari itapatikana, kwa hiyo uchunguzi wa suala hili ukamilike kwa haraka ili tupate ripoti itakayotusaidia muwekezaji aanze utaratibu wa kuanza uzalishaji ili wananchi waendele kupata bidhaa hiyo.” amefafanua Mhe Ndejembi.

Ametoa pole kwa wote waliopoteza ndugu zao na kuwahakikishia, Serikali kupitia Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa bega kwa bega na uongozi wa kiwanda tangu ajali ilipotokea ili kuhakikisha wote waliopoteza wapendwa wao wanapatiwa fidia.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma ameeema tayari timu ya wataalamu kutoka Mfuko huo imeanza mchakato wa kuwezesha wategemeza wa wafiwa wanapatiwa fidia kwa mujibu wa sheria.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usalama na Afya mahali pa Kazi, Bi Khadija Mwenda amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa ubadilishaji wa mfumo wa kuzalisha mvuke ndio uliopelekea tatizo hilo.

Aidha Mmiliki wa kiwanda hicho Bw Nassor Ali Seif, amesema tayari kiwanda kimeanza kuchukua hatua mbalimbali za muda mfupi na muda mrefu ili kuhakikisha kwamba tukio kama hilo halijitokezi