Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI 2021 YAKAMILIKA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kikao kilifanyika tarehe 29 Aprili, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo.Kauli Mbiu ya Mei Mosi 2021: “Masilahi Bora, Mishahara Juu, Kazi iendelee”

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Prof. Jamal Katundu (kulia) muonekano wa uwanja wa CCM Kirumba utavyokuwa, wakati wa kukagua maandalizi ya kuelekea sherehe za Wafanyakazi za Mei Mosi Jijini Mwanza, ukaguzi huo ulifanyika tarehe 29 Aprili, 2021.