Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Kikao kazi cha kuongeza Ufanisi Kwa Watumishi Idara ya kazi


Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Kazi imefanya Mafunzo kwa Watumishi wa Idara hiyo kutoka katika ofisi zake za mikoa , ambapo lengo la Mafunzo hayo ni kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu yao.

Mafunzo hayo ya kuwanoa maafisa kazi hao yamefanyika kuanzia tarehe 17 hadi 18 Oktoba, 2024 Mkoani Morogoro.

Kamishna mwenye dhamana ya masuala ya Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Suzan Mkangwa ameongoza mafunzo hayo ikiwa ni chachu ya ufanisi katika utekelezaji wa majukumu kwa Watumishi wa Idara ya Kazi.

"Kila mtumishi wa Idara ya Kazi hana budi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na kuhakikisha anafuata maadili ya Utumishi wa umma"