Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Mary Maganga asifu matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma PSSSF


KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga amesifu matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Bi. Maganga amesema hayo wakati akizungumza na Menejimenti ya PSSSF, alipotembelea Makao Makuu Ndogo ya PSSSF jijini Dar es Salaam Mei 29, 2024.

“Matumizi ya TEHAMA yanarahisisha utoaji wa huduma, niwapongeze kwa hatua ambayo mmeipiga,” alisisitiza.

Awali, Katibu Mkuu huyo alipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru ambaye alisema Mfuko unaendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Amesema, karibu shughuli zote za Mfuko zinaendeshwa kupitia mtandao.