Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Marry akitaka TLB kuzingatia sheria za Chama


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Marry Maganga ameshiriki katika kikao cha kupokea taarifa ya uchunguzi ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) leo Julai 2, 2024 , Dodoma.

Katika kikao hicho Maganga amewasihi wajumbe wa Chama hicho kuzingatia sheria za chama ili kuendeleza demokrasia na kuwa wawakilishi wazuri kwa wanao wawakilisha.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa TLB, Bi. Habiba Ngulangwa ameipongeza Serikali kwa kutoa ruzuku ya zaidi ya shilingi Milioni 19 kwa wasioona.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Zuhura Yunus na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu, Rasheed Maftah.