Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Maganga: Matumizi ya Mfumo wa kusajili migogoro kuepusha malalamiko na ucheleweshwaji haki


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mary Maganga amesema mfumo mpya wa kusajili migogoro ya kikazi kwa njia ya mtandao unaoratibiwa na CMAutasaidia kuepusha malalamiko na ucheleweshwaji wa haki kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi wa utendaji wa Tume hiyo.

Amesema hayo leo Julai 24, 2024 Jijini Dodoma, wakati akifungua mafunzo maalum ya mfumo wa kusajili migogoro ya kikazi unaofahamika kama ‘Online Case Management’ kwa watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Aidha, Katibu Mkuu Maganga amesema kuwa, matumizi ya mifumo yanaongeza ufanisi wa utendaji kwa namna mbalimbali na pia uwezo wa kutumika katika mazingira mbalimbali bila kuhitaji kwenda katika ofisi husika kupata huduma.

Vile vile, amewataka watumishi kuendelea kusimamia haki katika ajira na kazi kwa kuhakikisha wanatatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kwani ndio wajimu wao kwa Tume.

Kwa upande mwengine, Katibh Mkuu Maganga amepongeza CMA kwa kuendelea kusuluhisha migogoro ya kikazi hadi kufikia asilimia 76% ikiwa ni hatua nzuri kulingana na mpango mpango wa kuhakikisha wanafikia asilimia 81% kwa njia ya Usuluhishina hivyo kuonekana katika hatua inayoridhisha.

Naye, Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Usekelege Mpulla amesema mfumo huu unatarajiwa kutumika kutekeleza lengo la Tume ikiwa ni kuwafikia wadau mbalimbali kwa urahisi popote walipo.