Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Katibu Mkuu Maganga ahimiza uadilifu, weledi katika kuhudumia wananchi


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mary Maganga amewahimiza watumishi wa Ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kuzingatia taratibu na kanuni zilizopo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Katibu Mkuu Maganga amebainisha hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo Januari 6, 2024 Jijini Dodoma ambapo pia alipokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Ofisi hiyo kwa kipindi cha Julai hadi Desemba kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Aidha, amesema uwepo wa baraza la wafanyakazi unasaidia kuongeza ufanisi na tija katika sehemu za kazi na kutoa wasaa kwa waajiri na wafanyakazi kubadilishana mawazo na kubaini mbinu za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Awali akizungumza Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TUGHE Msumbisi Mwasandede ameipongeza Ofisi hiyo kwa kuhakikisha mabaraza ya wafanyakazi yanafanyika na kuhimiza Idara ya kazi iongezewe nguvu ili kuimarisha usimamizi wa sheria za kazi hususani sekta binafsi ili waajiri wazingatie viwango vya ajira.